Kozi ya bure · Kiswahili
Tumia AI kazini, kwa Kiswahili.
Video fupi na mazoezi kwenye simu yako: kuiomba AI vizuri, kuhakiki inachoandika, na kuitumia kazini. Na Haidari Gurumo wa Potiva Frontier Solutions.
Kwa makampuni: mafunzo ya AI kwa timu nzima →- 10
- masomo
- Bure
- kwa wote
- Kila wiki
- Jumamosi
Kozi ya bure · masomo 10
Masomo
Gusa namba kufungua somo hilo moja kwa moja. Masomo mapya hutoka kila Jumamosi.
Umeanza katikati? Hakuna shida. Anza na Somo la 1 hapa, au tazama yote kwa mpangilio kwenye orodha ya YouTube.
Jinsi inavyofanya kazi
Tazama. Jaribu. Tumia.
- 01
Tazama video
Dakika 4 hadi 6. Kila video inakuambia ni somo la ngapi.
- 02
Fanya mazoezi
Kadi fupi kwenye simu: tabiri, andika ombi, kamata makosa ya AI. Ulizokosa zinarudi siku zinazofuata.
- 03
Tumia kazini
Kila somo linaishia na kazi moja ya kufanya wiki hiyo.
Madarasa ya kulipia
Unataka kwenda mbali zaidi?
Madarasa madogo yenye mwalimu, kazi za vitendo na ukaguzi wa kazi yako. Kila darasa linajengwa juu ya kozi ya bure.
Kwa makampuni na taasisi
Unataka timu yako yote ijifunze hivi?
Kozi hii ni ya bure kwa kila mtu. Kwa makampuni, Potiva inaendesha mafunzo ya AI kwa timu nzima, kwa kazi zenu halisi, kwa Kiswahili au Kiingereza.
- Warsha ofisini kwenu au mtandaoni
- Sera ya matumizi salama ya AI ya kampuni yenu
- Kila mshiriki anafanya kazi moja halisi kwa AI
Msaada
Umekwama?
Majibu mafupi kwa matatizo ya kawaida kwenye simu.
Nitajiungaje na kundi la WhatsApp?
Bonyeza Jiunge na kundi la WhatsApp juu ya ukurasa huu. Itafungua WhatsApp na ujumbe tayari: andika jina lako na utume. Tutakuunganisha kwenye kundi.
Kwenye kundi tunashirikiana maombi bora, maswali, na kazi za kila wiki.
Kufungua akaunti ya ChatGPT au Gemini
Njia rahisi ni akaunti yako ya Google, ile ile ya Play Store. Fungua app au tovuti (chatgpt.com au gemini.google.com), bonyeza kitufe cha kuingia, kisha chagua Google.
Simu haina nafasi? Tumia kivinjari badala ya app.
Menyu ziko kwa Kiingereza
Maneno ya kawaida:
- New chat: chat mpya
- Settings: mipangilio
- Personalization / Customize: maelekezo ya kudumu
- Memory: kumbukumbu
- Upload / Attach: pakia faili au picha
- Send: tuma
Unaweza pia kuiandikia AI kwa Kiswahili hata kama menyu ni za Kiingereza.
AI imesema nimefikia kikomo
Matoleo ya bure yana kikomo cha ujumbe au cha zana fulani kwa muda fulani. Subiri muda unaotajwa, au endelea na zana nyingine kwa kazi hiyo hiyo. Ndiyo sababu ni vizuri kujua zana mbili.
Data: kiasi gani?
Kila video imeandikwa ukubwa wake (MB) kwenye somo. Mazoezi ni madogo sana, na yakishafunguka mara moja yanafanya kazi hata bila mtandao.
Kupakia picha au PDF kwenye AI kunatumia data zaidi kuliko kuandika. Tumia Wi-Fi ukiweza.
Maendeleo yangu yamepotea
Bila akaunti, maendeleo yanahifadhiwa kwenye kivinjari cha simu hii tu. Ukifuta data ya kivinjari, au ukifungua kwenye kivinjari kingine, hayaonekani.
Tumia namba ya nakala kwenye Mradi wangu kuhamisha maendeleo yako kwenye simu nyingine.
Kurudia, na streak, vinafanyaje kazi?
Kadi ulizokosa zinarudi kesho. Ulizopata zinarudi baada ya siku 2, kisha 7, kisha 21. Hivyo ndivyo kumbukumbu inavyodumu.
Siku inahesabika ukijibu kadi moja tu. Ukikosa siku moja kwa wiki, streak haikatiki.